Usiku wa leo kunatarajiwa kuonekana mwezi mkubwa unaotambulika na wanasayansi kama 'Super Moon'.
Mwezi huo pia utakuwa na mwonekano wa karibu zaidi kutoka angani .
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na shirika la masuala ya anga ya Marekani,NASA ni kuwa tukio hilo si la kihistoria la mwaka 2016 pekee bali pia ni historia kuu ya karne ya 21.
Aidha pia wanasayansi wanadai kuwa muonekano huo wa karibu wa mwezi uliwahi kutokea miaka 70 iliyopita.
Vilevile muonekano huo wa karibu hautaonekana tena hadi mwezi Novemba 24 mwaka 2034.
Baada ya miaka 68 kwa mara ya kwanza utaonekana kwa ukubwa wa asilimia 14 zaidi huku mwanga ukiongezeka kwa asilimia 30 zaidi.

No comments:
Post a Comment