
MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta anayekipiga klabu ya TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amepata ofa nne za kujiunga
na klabu mbalimbali barani Ulaya.
Akizungumza
na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Samatta alisema nchi
karibu nne zimemfuata na kuonyesha nia ya kumtaka, lakini bado
anatafakari.
Samatta
nyota aliyetimkia Mazembe akitokea klabu ya Simba ya Tanzania, alisema,
tayari ameshautaarifu uongozi wake wa klabu yake juu ya ofa hizo,
lakini wasiwasi wake ni nafasi ya kuachiwa kwake na timu hiyo ambayo
bado ana mkataba nao wa msimu mmoja.
Timu
hizo na nchi ziliko sitoweza kuzitaja kwa sasa, mambo yatakapokaa sawa
nitaweka wazi kila kitu, si unajua tena. Lakini nina wasiwasi, sijui
kama uongozi wa timu yangu watakubali niondoke kutokana na mchango wangu
katika timu hiyo
alisema Samatta.
Aliongeza
kuwa anawafahamu viongozi wake kuwa ni waelewa, hivyo basi wakati
ukifika anamuomba Mungu amtangulie ili aweze kuruhusiwa kwenda kutimiza
ndoto zake barani Ulaya
Source
No comments:
Post a Comment